KCMC NA TUMBI WAWEKA NGUVU PAMOJA
Hospitali ya KCMC leo imepokea ugeni kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani, Tumbi, http://instagram.com/hospitali_ya_tumbi ukiongozwa na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt. Aman Malima, akiambatana na watumishi mbalimbali.
Ziara hiyo ya kikazi imelenga kujengeana uwezo na kubadilishana uzoefu katika maeneo muhimu ya utoaji wa huduma za afya pamoja na mafunzo.
Katika ziara hiyo, ujumbe kutoka Tumbi umepata fursa ya kujifunza kutoka KCMC kuhusu mifumo na uzoefu wa hospitali katika kuboresha huduma kwa wagonjwa, kuendeleza mafunzo kwa wataalamu wa afya ili kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya afya.
Aidha, ziara hiyo imekuwa fursa muhimu kwa watumishi wa hospitali hizi mbili kushirikishana uzoefu, maarifa na mbinu bora za utendaji, huku wakijadili maeneo ambayo yanaweza kuendelezwa kupitia ushirikiano wa kitaalamu.
Uongozi wa KCMC umeeleza kuwa ushirikiano na hospitali nyingine ni muhimu katika kujifunza, kubadilishana uzoefu na kujenga uwezo wa watumishi, kwa lengo la kuongeza ufanisi na ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Related Stories