Processing...

News Room

JUMUIYA YA WANAWAKE KATIKA NYUKLIA TANZANIA YAZURU KCMC

JUMUIYA YA WANAWAKE KATIKA NYUKLIA TANZANIA YAZURU KCMC
JUMUIYA YA WANAWAKE KATIKA NYUKLIA TANZANIA YAZURU KCMC
JUMUIYA YA WANAWAKE KATIKA NYUKLIA TANZANIA YAZURU KCMC
+3 More Images
JUMUIYA YA WANAWAKE KATIKA NYUKLIA TANZANIA YAZURU KCMC
JUMUIYA YA WANAWAKE KATIKA NYUKLIA TANZANIA YAZURU KCMC
Women in Nuclear Tanzania, chini ya Tanzania Atomic Energy Cammission (TAEC), wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini - KCMC, katika Idara ya Watoto Wenye Saratani, na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa watoto wanaoendelea kupatiwa matibabu. Mbali na kutoa msaada huo, Women in Nuclear Tanzania walipata fursa ya kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ya hospitali pamoja na kuwa na mazungumzo ya kupeana elimu kuhusu mionzi ya nyuklia (nuclear radiation), matumizi yake na faida zake, hasa katika sekta ya afya. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Bi. Hellen Emmanuel, Mtaalamu wa Maabara kutoka Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), alieleza umuhimu wa wanawake wanasayansi kuwa na uelewa wa sayansi na teknolojia ya nyuklia, akibainisha kuwa elimu hiyo inawawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika maeneo mbalimbali ya matumizi ya teknolojia ya nyuklia, ikiwemo huduma za afya, utafiti, viwanda na sekta nyingine muhimu kwa maendeleo ya Tanzania. Aidha, alieleza kuwa uelewa sahihi kuhusu teknolojia ya nyuklia unasaidia jamii kufahamu matumizi yake, manufaa yake pamoja na umuhimu wa kuzingatia usalama katika matumizi ya mionzi. Ziara hiyo pia imelenga kuimarisha na kuendeleza ushirikiano kati ya Women in Nuclear Tanzania na KCMC, huku ikitoa nafasi ya kuwafariji na kuwapa matumaini wagonjwa wa saratani, zaidi kwa watoto wanaoendelea na matibabu katika Hospitali ya Kanda ya Kaskazini KCMC. KCMC inatoa shukrani kwa Women in Nuclear Tanzania na Tanzania Atomic Energy Agency kwa kuendelea kushirikiana na hospitali na kuwa sehemu ya jitihada za kutoa faraja, matumaini na msaada kwa watoto wenye saratani.

Related Stories

JUMUIYA YA WANAWAKE KATIKA NYUKLIA TANZANIA YAZURU KCMC
2026-08-13 00:00:00

JUMUIYA YA WANAWAKE KATIKA NYUKLIA TANZANIA YAZURU KCMC

READ ARTICLE
SNAKE ANTIVENOM ZAFIKA KCMC
2026-08-13 00:00:00

SNAKE ANTIVENOM ZAFIKA KCMC

READ ARTICLE
WATAALAMU WA DIALYSIS WAHITIMU KCMC
2026-08-13 00:00:00

WATAALAMU WA DIALYSIS WAHITIMU KCMC

READ ARTICLE

Join the Discussion

× Preview
🫀
CHANGIA JENGO LA MOYO
Saidia Ujenzi wa Cardiovascular Centre