WATAALAMU WA DIALYSIS WAHITIMU KCMC
Hospitali ya KCMC imeandika historia nyingine katika safari yake ya kuimarisha na kuboresha huduma za afya nchini, baada ya wanafunzi wa Kozi ya Uchujaji Damu kwa Mashine (Dialysis) kukamilisha mafunzo yao ya miezi mitatu na kukabidhiwa vyeti vyao vya kuhitimu.
Mafunzo hayo yalizinduliwa rasmi tarehe 12 Mei 2026, yakiongozwa na Mtaalamu Bingwa wa Magonjwa ya Figo - KCMC, Dkt. Huda Akrabi, kwa lengo la kuwajengea uwezo wataalamu wa afya katika kutoa huduma salama, bora na zenye kuzingatia viwango vya kitaalamu za Hemodialysis.
Kozi hiyo iliwakutanisha wahudumu wa afya kutoka maeneo mbalimbali nchini, wakiwemo Bukoba, Musoma na Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya jitihada za KCMC katika kusambaza ujuzi na uzoefu wa kitaalamu na kuchangia uimarishaji wa huduma za figo katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Baada ya kukamilisha mafunzo hayo, wahudumu hao wanarejea katika vituo vyao wakiwa wameongezewa maarifa, ujuzi na stadi za kitaalamu zitakazowawezesha kutoa huduma bora zaidi kwa wagonjwa wanaohitaji matibabu ya Hemodialysis.
Related Stories