Processing...

2026-04-21 00:00:00 MOYO 5 min read

TUTATULIZA WATU MIOYO

Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini – KCMC kwa kushirikiana na uongozi wa TANLINK leo umetembelea ofisi za Crown Media zilizopo Mikocheni, Dar es Salaam, na kufanya mazungumzo ya pamoja na uongozi wa taasisi hiyo. Lengo kuu la ziara hii ni kuimarisha ushirikiano katika upande wa mawasiliano na uelimishaji wa umma, ili kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu namna bora ya kuchangia ujenzi wa Taasisi ya Moyo ya KCMC. Kupitia jukwaa la vyombo vya habari, Crown Media inatarajiwa kuwa kiungo muhimu katika kufikisha ujumbe huu kwa jamii kwa upana zaidi. Ujenzi wa Taasisi ya Moyo ya KCMC ni mradi muhimu unaolenga kuboresha huduma za matibabu ya moyo nchini, na mafanikio yake yanategemea mshikamano na ushiriki wa wadau wote, ikiwemo wananchi. KCMC inaendelea kuhamasisha jamii kujitokeza kuchangia mradi huu wa kihistoria, kwani kila mchango ni hatua ya kuokoa maisha. https://www.instagram.com/p/DXY-hWliO0k/?igsh=bHhicGh6OGZud3Jp

Related News

Medical technology
2026-04-21 00:00:00

PIGO MOJA LA MOYO NI UHAI

Read Story →
Medical technology
2026-04-21 00:00:00

TUTATULIZA WATU MIOYO

Read Story →
Medical technology
2026-04-21 00:00:00

DKT. URASA AHAMASISHA UPIMAJI WA AFYA

Read Story →

Leave a Comment

🫀 CHANGIA JENGO LA MOYO