SIKU IMEWADIA
Hatimaye siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imewadia! 🇹🇿
shamrashamra zinaendelea hapa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini – KCMC, huku kila kitu kikiwa tayari kwa kumpokea mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ni siku ya kihistoria kwa KCMC na kwa sekta ya afya nchini, tunaposubiri kwa hamu kuanza kwa tukio hili muhimu litakaloandika ukurasa mpya katika utoaji wa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi kwa Watanzania.
Karibu KCMC, Mhe. Rais.
#KCMC #KaribuKCMC #SamiaSuluhuHassan #AfyaBora #Tanzania
Related Stories