Processing...

News Room

IDARA YA WATOTO KCMC YAPATA TUZO

IDARA YA WATOTO KCMC YAPATA TUZO
IDARA YA WATOTO KCMC YAPATA TUZO
IDARA YA WATOTO KCMC YAPATA TUZO
+3 More Images
IDARA YA WATOTO KCMC YAPATA TUZO
IDARA YA WATOTO KCMC YAPATA TUZO
Leo, tarehe 10 Agosti 2026, Hospitali ya KCMC kupitia Idara ya Watoto (Paediatric Department) imepokea tuzo ya pongezi kutoka katika Mradi wa NEST360, unaotekelezwa chini ya uongozi wa Ifakara Health Institute (IHI). Tuzo hiyo imelenga kupongeza juhudi na kazi kubwa inayofanywa na Idara ya Watoto ya KCMC katika kulinda uhai wa watoto, kupunguza vifo vya watoto na kuhakikisha kila mtoto anapata mwanzo salama wa maisha. Akizungumza wakati wa kukabidhi tuzo hiyo, Program Coordinator wa Mradi wa NEST360, Ndugu Allen Kinyina, alipongeza juhudi kubwa zinazofanywa na uongozi wa KCMC kupitia Idara ya Watoto katika kuimarisha huduma za afya kwa watoto. Alisema juhudi hizo zimekuwa na mchango mkubwa katika kupunguza vifo vya watoto, pamoja na kuhakikisha watoto wanaozaliwa wanapata huduma muhimu kwa wakati, ikiwemo kuanzishiwa unyonyeshaji mapema na kupata huduma stahiki zinazowawezesha kukua katika afya bora. Tuzo hiyo ni ishara ya kutambua na kuthamini kujitolea kwa wataalamu wa Idara ya Watoto KCMC katika kuhakikisha kila mtoto anayezaliwa anapata huduma bora, salama na yenye kuzingatia uhai na afya yake. https://www.instagram.com/p/Db2pJ4uAhbR/?igsh=MW00c3ZhNGV2eW44NQ==

Related Stories

IDARA YA WATOTO KCMC YAPATA TUZO
2026-08-10 00:00:00

IDARA YA WATOTO KCMC YAPATA TUZO

READ ARTICLE
KCMC YATATHIMINI MPANGO MKAKATI 2022-2026
2026-08-06 00:00:00

KCMC YATATHIMINI MPANGO MKAKATI 2022-2026

READ ARTICLE
25 KCCO ANIVERSARY
2026-08-06 00:00:00

25 KCCO ANIVERSARY

READ ARTICLE

Join the Discussion

× Preview
🫀
CHANGIA JENGO LA MOYO
Saidia Ujenzi wa Cardiovascular Centre