2026-04-09 00:00:00
•
Afya Ya Moyo
•
5 min read
KMC YAZINDUA KAMPENI YA UCHANGIAJI WA JENGO LA MATIBABU YA MOYO
Mapema leo tarehe 09 aprili 2026 katika Hoteli ya Johari Rotana, Dar es Salaam, Uongozi wa Hospitali ya KCMC umefanya mkutano na waandishi wa habari kutangaza rasmi kampeni ya uchangiaji wa ujenzi wa Jengo la Matibabu ya Moyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC, Prof. Gileard Masenga, ameongoza mkutano huu nakueleza kuwa magonjwa ya moyo yanaendelea kuwa tishio kubwa, yakichangia idadi kubwa ya vifo duniani na hapa nchini. Ndani ya KCMC pekee, wagonjwa wa moyo ni sehemu kubwa ya wanaolazwa na baadhi yao hulazimika kulazwa mara kwa mara, hali inayoonesha ukubwa wa changamoto.
Kutokana na hali hiyo, KCMC imeanzisha mradi wa kujenga kituo cha kisasa cha moyo kitakachotoa huduma zote muhimu ikiwemo uchunguzi, matibabu ya kisasa na upasuaji wa moyo. Lengo ni kupunguza rufaa za nje ya nchi na kuokoa maisha ya Watanzania wengi zaidi.
Mradi huu unatarajiwa kugharimu takribani shilingi bilioni 50 (bilioni 25 ujenzi na bilioni 25 vifaa) ambapo tayari wadau wa kimataifa wamejitolea kufadhili sehemu kubwa ya gharama. Hata hivyo, mchango wa Watanzania bado ni muhimu ili kufanikisha azma hii kubwa ya kitaifa.
Kupitia mkutano huu, KCMC imetoa wito kwa Watanzania wote ndani na nje ya nchi kuungana katika juhudi hizi za kuokoa maisha.
Kila mchango ni muhimu. Kila mchango ni uhai.
Tuchangie leo, tuokoe maisha kesho.
#KCMC #AfyaYaMoyo #Tanzania #SaveLives
Related News
2026-04-01 00:00:00
MAPAMBANO DHIDI YA SARATANI YASHIKA KASI: KCMC YAZINDUA KAMATI MAALUM
Read Story →