KUTANA NA KCMC `BAKWATA KILIMANJARO`
KCMC kupitia maabara yake ya kisasa (KCMC Centre of Excellence Laboratory,CoE) @kcmc_coe , leo inaendelea kutoa huduma za vipimo vya afya bure kwa wananchi katika ofisi za BAKWATA Mkoa wa Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kujua hali ya afya zao na kufanya uchunguzi wa afya kwa wakati.
Huduma hii imevutia viongozi mbalimbali, akiwemo Mbunge wa Moshi Mjini, Mheshimiwa Ibrahimu Shayo, ambaye amesisitiza umuhimu wa wananchi kufanya vipimo vya afya mara kwa mara na kuwataka kutumia fursa hii adhimu ya kupata huduma za uchunguzi wa afya bila malipo.
Aidha, Sheikh Mkuu wa BAKWATA Mkoa wa Kilimanjaro, Sheikh Shaban Mlewa, amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi, pamoja na kuwashawishi wengine kushiriki katika huduma hii. Amewasisitiza wananchi kutokuwa na hofu ya kupokea majibu ya vipimo, kwani kujua hali ya afya ni hatua muhimu katika kujikinga na kutafuta matibabu kwa wakati.
Vipimo vinavyotolewa bure ni: Presha(bp), Sukari ya damu (RBG na HbA1c), Utendaji kazi wa figo, Utendaji kazi wa ini, Mafuta kwenye damu (Cholesterol), Uzito na urefu, Mzunguko wa kiuno
Pamoja na vipimo hivyo, washiriki wanapata elimu ya afya, na pia kuna fursa ya kuchangia damu kwa wale watakaokuwa tayari.
KCMC Centre of Excellence inaendelea kuunga mkono juhudi za kuimarisha afya ya jamii kwa kuleta huduma za uchunguzi, elimu na uhamasishaji karibu na wananchi.
Afya ni utajiri. Jitokeze kupima, jua hali yako ya afya, na chukua hatua mapema!
#KCMC #KCMCCentreOfExcellence #AfyaKwaJamii #Kilimanjaro #HudumaZaAfya
Related Stories