Processing...

News Room

KUTOKA SWEDEN HADI KCMC

KUTOKA SWEDEN HADI KCMC
KUTOKA SWEDEN HADI KCMC
KUTOKA SWEDEN HADI KCMC
+8 More Images
KUTOKA SWEDEN HADI KCMC
KUTOKA SWEDEN HADI KCMC
KUTOKA SWEDEN HADI KCMC
KUTOKA SWEDEN HADI KCMC
KUTOKA SWEDEN HADI KCMC
KUTOKA SWEDEN HADI KCMC
KUTOKA SWEDEN HADI KCMC
Hospitali ya KCMC imepokea wageni kutoka Dayosisi ya Stockholm nchini Sweden, wakiwemo Wachungaji, Mashemasi, wanamuziki wa kanisa pamoja na waumini, wakiwa sehemu ya kundi linalowakilisha zaidi ya sharika 10 za dayosisi hiyo. Katika ziara hiyo, wageni hao wametembelea KCMC pamoja na Kituo cha Ushauri na Utunzaji Kichungaji (CPE), kwa lengo la kujifunza na kujionea namna huduma mbalimbali za afya na huduma za kichungaji zinavyotolewa kwa wagonjwa na jamii kwa ujumla. Ziara hiyo imekuwa fursa kwa wageni hao kupata uelewa wa shughuli zinazofanywa na KCMC, mifumo ya utoaji huduma pamoja na mchango wa huduma za kichungaji katika kuwasaidia wagonjwa na familia zao kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiafya na kijamii. Kupitia ziara hiyo, wageni wamepata nafasi ya kujifunza kuhusu namna huduma za afya na huduma za kiroho zinavyoweza kwenda sambamba katika kutoa huduma inayomjali mgonjwa kwa ukamilifu, ikizingatia mahitaji yake ya kimwili, kisaikolojia na kiroho. Ziara hiyo pia ni sehemu ya kuimarisha mahusiano, kubadilishana uzoefu na kujenga uelewa wa pamoja kuhusu nafasi ya taasisi za afya na kanisa katika kuhudumia binadamu.

Related Stories

KUTOKA SWEDEN HADI KCMC
2026-11-17 00:00:00

KUTOKA SWEDEN HADI KCMC

READ ARTICLE
WAJUMBE WA BARAZA LA GSF WAJIONEA MIUNDOMBINU YA HOSPITALI
2026-11-06 00:00:00

WAJUMBE WA BARAZA LA GSF WAJIONEA MIUNDOMBINU YA HOSPITALI

READ ARTICLE
KCMC NA WADAU WA AFYA WAIMARISHA USHIRIKIANO KUPITIA MRADI WA FCI
2026-11-06 00:00:00

KCMC NA WADAU WA AFYA WAIMARISHA USHIRIKIANO KUPITIA MRADI WA FCI

READ ARTICLE

Join the Discussion

× Preview
🫀
CHANGIA JENGO LA MOYO
Saidia Ujenzi wa Cardiovascular Centre