KCMC YAENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA HOSPITAL KANDA ZA KASKAZINI
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini – KCMC imeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuwakutanisha viongozi wa hospitali na watumishi wa afya kutoka hospitali za Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya.
Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa KCCO – KCMC, umefunguliwa na kuongozwa na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa KCMC, Dkt. Ayesiga Herman (picha ya 8).
Katika mkutano huo, wadau wa sekta ya afya kutoka taasisi mbalimbali wamejadili masuala muhimu yanayohusu utoaji wa huduma bora za afya, mikakati ya kuboresha utendaji kazi, pamoja na kujengeana uwezo katika maeneo mbalimbali ya kitaalamu.
Mikutano hii inayofanyika mara mbili kwa mwaka inalenga kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi za afya, kuhamasisha ubadilishanaji wa maarifa na uzoefu, pamoja na kujenga mtandao imara wa kitaalamu unaochangia kuboresha huduma za afya kwa wananchi katika Kanda ya Kaskazini.
Related Stories
2026-10-16 00:00:00
KCMC YAENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA HOSPITAL KANDA ZA KASKAZINI
READ ARTICLE