13-03-2026 10:34:27
•
BAJETI
•
1 min read
BAJETI YA 2026/2027 YAWAKUTANISHA
Menejimenti ya Hospitali ya KCMC leo imeketi pamoja na Kamati ya Bajeti katika kikao kilicholenga kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027. Kikao hicho kimefanyika kwa lengo la kujadili bajeti iliyowasilishwa na kamati hiyo, pamoja na kutoa nafasi kwa wajumbe wa menejimenti ya hospitali kuchangia mawazo, maoni na ushauri utakaosaidia kuboresha na kuimarisha mpango huo wa kifedha.
Katika kikao hicho, viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo Wakurugenzi, Wakuu wa Idara, vitengo na Waratibu walipata fursa ya kuchambua vipaumbele vilivyowekwa katika bajeti hiyo, sambamba na kujadili shughuli na miradi mbalimbali inayolenga kuendeleza huduma zinazotolewa na hospitali. Aidha, wajumbe walitoa mapendekezo mbalimbali yaliyolenga kuhakikisha bajeti hiyo inaendana na mahitaji halisi ya hospitali pamoja na kuimarisha ufanisi katika matumizi ya rasilimali zilizopo.
Related News