Processing...

2026-02-28 00:00:00 MICHEZO 5 min read

KCMC NA REKODI NYINGINE: MICHEZO 6 YASHNDA MICHEZO 5

Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Hospitali ya KCMC imeandika historia ya kuwa ya kwanza kushinda michezo mi 5 mfululizo kati ya 6. Hii ni ishara ya nidhamu, mshikamano na kujituma kwa hali ya juu kutoka kwa wachezaji na benchi la ufundi. Ushindi huu unathibitisha kuwa KCMC sio tu bora katika huduma za afya bali pia katika michezo ya kujenga afya ya mwili. Aidha, katika michezo hiyo sita KCMC imeshinda kama ifuatavyo: ⚽ Mpira wa Miguu: KCMC nafasi ya kwanza, huku Rombo District Council (Rombo DC) wakishika nafasi ya pili. 🏐 Mpira wa Pete: KCMC nafasi ya kwanza, Rombo DC nafasi ya pili. 🏐 Mpira wa Wavu (Volleyball): KCMC nafasi ya kwanza, Rombo DC nafasi ya pili. ♟ Draft (Mchezo wa Jadi): KCMC nafasi ya kwanza, Rombo DC nafasi ya pili. 🃏 Karata: KCMC nafasi ya kwanza, Rombo DC nafasi ya pili. 🎱 Pool Table: KCMC nafasi ya pili, huku Rombo DC wakichukua nafasi ya kwanza. Katika kupongeza juhudi hizo timu za mipira zilizoibuka washindi wa kwanza zimepewa makombe huku washindi wa kwanza upande wa michezo ya jadi wakipewa medali. Kwa matokeo haya, KCMC imeonesha ubora na ushindani wa hali ya juu katika karibu kila mchezo, ikithibiti sha kuwa ni taasisi imara ndani na nje ya majukumu yake ya kiafya.

Related News

Medical technology
2026-04-09 00:00:00

KMC YAZINDUA KAMPENI YA UCHANGIAJI WA JENGO LA MATIBABU YA MOYO

Read Story →
Medical technology
2026-04-01 00:00:00

MAPAMBANO DHIDI YA SARATANI YASHIKA KASI: KCMC YAZINDUA KAMATI MAALUM

Read Story →
Medical technology
2026-03-24 00:00:00

MAPAMBANO DHIDI YA LISHE DUNI

Read Story →

Leave a Comment

🫀 CHANGIA JENGO LA MOYO