Kinu cha kufua na kutengeneza hewa ya oksijeni na nitrojeni (Oxgen and Nitrogen plant)

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa KCMC, DKt.Gileard Masenga ameongoza Wafanyakazi na Wachungaji wa KCMC 30/11/2018 Kuzindua ujenzi wa Kinu cha kufua na kutengeneza hewa ya oksijeni na nitrojeni (Oxgen and Nitrogen plant) kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa.Kinu hicho kitakuwa na uwezo wa kufua na kujaza hewa ya Oksijeni na nitrojeni kwa mitungi mia nne (400) kwa muda wa masaa ishirini na nne(24) tu.