|
Sisi
tu nani
Tunafanya kazi gani
Tunawatembelea wagonjwa waliolazwa, na wanaofika kwa matibabu bila
kulazwa.
Tunaingiza ibada katika kikanisa cha Hagai hapa hospitalini kila
Jumapili saa 2 (kwa Kiingereza) na saa 4 (kwa Kiswahili).
Tunaongoza sala ya asubuhi kwa watumishi wote wa KCMC pamoja na
wageni Jumatatu hadi Ijumaa saa 1 na nusu.
Tunapeleka Chakula cha Bwana kwa wagonjwa wodini ikiwa haja ipo.
Tunapeleka huduma za dharura kama vile ubatizo, kurudi kundini,
kupakia mafuta ikiwa haja ipo.
Wachungaji wetu
Mch. Archiboldy Lyimo (Kanisa la Kilutheri), Mkuu wa Idara
Mch. John Safari (Kanisa la Kilutheri)
Mch. Prince Hiiti (Kanisa la Kianglikan)
Fr. Salutaris Mawazo (Kanisa la Roman Catholic)
Mchungaji Mgeni
Mch. Dk. Günter Kohler (Kanisa la Kilutheri, toka Ujerumani)
Wahudumu wengine
P/W Frida Kitange
Karani Joyce Lyatuu
Mhudumu Mgeni
Maja Kohler (Ustawi wa jamii, toka Ujerumani)
Tuko wapi
Idara ya wachungaji ni kwenye ghorofa
la chini. Unapoingia kutoka mbeleni upitie mapokezi ya wanaolazwa,
ukate kushoto. Unapofika mwisho wa njia hii uzunguke hatua chache
upande wa kushoto; kipo kibao kinachoonyesha “Uchunguzi wa
Matatizo”. Ukikata kulia tupo hapo, kuingia kwenye mlango
“G15”.
Tunaweza kuitwa kwa kupitia mtunza
simu wa hospitali (namba 133 au 131).
Link CPE
Mawasiliano
K.C.M.C. Idara ya Uchungaji
S.L.P. 545
Moshi, Tanzania
Simu: (+255) ………
Barua pepe: JohnsonKCMC@yahoo.com
|
About us
What we do
We visit the patients admitted to the wards, and also the outpatients.
We have services in the Hagai hospital chapel on Sundays at 8 a.m.
(English), and at 10 a.m. (Kiswahili).
Every morning from Monday to Friday we have morning devotion in
the Chapel for hospital staff as well as for patients at 7:30 a.m.
We provide the Lord’s Supper to patients on the wards upon
request.
We render emergency services like baptism, ointment of the sick
or last rites upon request.
Our ministers:
Rev. Archibold Lyimo (Lutheran), Head of Department
Rev. John Safari (Lutheran)
Rev. Prince Hiiti (Anglican)
Fr. Salutaris Mawazo (Roman Catholic)
Guest minister
:
Rev. Dr. Günter Kohler (Lutheran, from Germany)
Other staff :
Frida Kitange, Parish Worker
Joyce Lyatuu, Secretary
Guest staff:
Maja Kohler, (Social Worker, from Germany)
How to Reach Us
The chaplaincy department is located
on the ground floor. Coming from the front entrance you pass through
the reception area of the admitted patients, then turn left. At
the end of the pass-way you turn just a bit left until you see a
sign “Uchunguzi wa Matatizo – Clearing of Problems”.
Turn right and find us there, entering the “G15” door.
We can always be called by the telephone
operator of the hospital (ext. 133 or 131).
Link ? CPE
Contact us
K.C.M.C. Chaplaincy Office
P.O.B. 545
Moshi, Tanzania
Phone: (+255) ………….
E-mails:
JohnsonKCMC@yahoo.com |
Kozi ya Ushauri
wa Kichungaji na Ushauri Nasaha
( CPE )
Dira na taswira / kusudi
Kozi ya CPE hapa K.C.M.C., Moshi, inatoa mafundisho
ya utunzaji na ushauri wa kichungaji kwa wachungaji na watu wenye
uzoefu katika ustawi wa jamii, katika mafunzo ya afya na katika
uongozi wa hospitali hapa Tanzania na katika nchi nyingine za Afrika
ya Mashariki.
Mkazo umewekwa hasa kwa ushauri nasaha wa kiroho
kwa watu wanaopambana na matatizo yanayoletwa na ukimwi.
Msingi wa CPE katika maeneo yote ya kazi zilizotajwa hapa juu ni
kuangalia hali ya kiroho ya mtu. Hivyo kozi za CPE zinaingiza baraka
maalum kutoka Injili katika kazi za makanisa, za jamii, za vituo
vya afya na za udiakonia.
Tunawakaribisha wanafunzi kutoka madhehebu yote
ya kikristo.
Namna ya kufundisha CPE
CPE ni mtindo wa mafundisho unaojenga juu ya uzoefu
na utendaji. Utunzaji na ushauri wa kichungaji unafundishwa na kuzoezwa
katika kutenda, na, wakati hali nzima ya mwanafunzi inapoguswa,
unaendelezwa katika mwanga wa theologia na saikolojia. Neno “Clinical”
hapa ina maana ya “katika utendaji” au “kuhusu
matatizo ya mtu“.
Wagonjwa waliolazwa K.C.M.C. ni “nyaraka hai
za kibinadamu” wetu wanaotufundisha jinsi a kutambua misingi
ya maisha ya binadamu, na jinsi ya kuhusanisha maisha ya mtu na
imani yake.
Kipengele cha ushauri nasaha
Sehemu ya majuma matatu ya kozi ya CPE imewekwa
kwa kuwapa wanafunzi ujuzi hasa na maarifa ili waweze kutoa ushauri
nasaha katika maeneo yao ya kazi.
Wakati wa mafundisho hayo ya ushauri nasaha tunashirikiana
na watumishi wa hospitali waliopitia mafunzo maalum kwa ajili ya
kazi hiyo. Tunatoa cheti (vilevile tunashughulika ili cheti hicho
kitambuliwe pia na wizara ya afya kwa kupitia National AIDS Counselling
Programme (NACP).
Walimu wa CPE
Mch. Archiboldy, Mkuu wa Chuo
Mch. John Safari
Mch. Prince Hiiti
Mch. Dk. Günter Kohler, Supervisor DGfP
Masharti ya kujiunga na kozi ya CPE
Fomu za kuomba kujiunga na kozi ya CPE inapatikana katika Idara
ya Uchungaji ya K.C.M.C.
Lugha ya kozi ya CPE
Lugha ya kozi kwa kazi zote za midomo na uandishi ni Kiswahili.
|
CPE Course including HIV/AIDS
Counselling
Mission and Vision of CPE
The CPE course at K.C.M.C., Moshi, provides for
education in pastoral care and counselling for ministers and other
professionals of the social welfare, health care, and hospital administration
sectors from Tanzania and other East African countries.
Particular attention is given to counselling and
pastoral care for HIV/AIDS afflicted persons. [Link to HIV/AIDS
part]
The spiritual aspect in all areas of work as cited above is the
base for CPE. The CPE courses thus provide for a fruitful input
from the Gospel to church related, social, health care, and diaconic
activities in society.
The courses are open for students from all Christian
denominations.
Teaching Method
CPE is an experience based method of learning in
which Pastoral Care and communication are learned and trained in
practice and, under the auspices of personality orientation, are
reflected from the viewpoints of theology, and human psychology.
The word “Clinical”, in this aspect, means “practice
oriented”, or “related to cases”.
The patients admitted to K.C.M.C. are our “living
human documents” from whom we learn to take a look at the
conditions of human life, and how to integrate life and faith.
HIV/AIDS Counselling
A three (four) weeks part of the course is designed
to furnish the students with the particular background knowledge
and skills to do HIV/AIDS counselling in their respective area of
work.
In this part of the course we cooperate with the
hospital staff trained for HIV/AIDS counselling. We issue a certificate
(we work on having our certificate recognized by the Ministry of
Health through the National AIDS Counselling Programme (NACP).
Teaching Staff
Rev. Archibold Lyimo, Head of CPE College
Rev. John Safari
Rev. Prince Hiiti
Rev. Dr. Günter Kohler, Supervisor DGfP
Admission Requirements
A form to request admission to the CPE course is available at the
Chaplaincy Department of K.C.M.C.
Course Language
The course language for all oral and written work is Swahili.
|